Member-only story

Carol Ndosi
5 min readFeb 23, 2020

Vijana na Ubunifu, Ujuzi, na Maarifa kwenye Soko la Ajira, Ujasiriamali na Kazi.

Tumekua tukilalama kuhusu changamoto ya ajira na kazi inayo wakabili vijana ambao ni kundi kubwa kuliko yote Tanzania. Imethibitishwa kuwa wastani wa umri wa Kijana kwa sasa Tanzania ni miaka 17.7.

Wengi wamekua wakihoji kama tumetanabaisha maana ya hizi takwimu na jinsi gani kama taifa tumejitayarisha kuendana na wimbi hili la vijana.

Wengi pia wamekua wakitoa angalizo la hitaji kubwa la mapinduzi ya mfumo wa elimu yatakayo hakikisha mitaala inatayarisha vijana kwa kuwapa elimu itakayo wawezesha kushiriki kikamilifu na kuwa washindani kwenye soko la ajira la sasa.

Kabla sijaangaza zaidi kwenye hili naomba kutanguliza kwanza msisitizo wa rai ya kuangalia fursa zilizopo kwenye kila changamoto tunayo kabiliana nayo. Ajira hazitoshi NDIO, takwimu zimethibitisha hivi kwa kuainisha kuwa idadi ya ajira imezidiwa na idadi ya vijana wanaoingia rasmi kwenye soko la ajira (wanaofikisha umri wa kujiajiri au kuajiriwa pamoja na wahitimu wa ngazi mbali mbali za elimu).

Hata tukisema tuangalie ajira zisizo rasmi kwenye sekta mashuhuri, maendeleo endelevu yanaendelea kuwa changamoto kwani ajira hizi zinatoa riziki ya mkono kwenda mdomoni tu yaani ‘hand to mouth’ na hivyo kuacha nafasi duni sana za kuzingatia mahitaji mengine ya kibinadamu na kijamii.

Ni kutokana na sababu hizi ndio maana tunaendelea kuwa na mzunguko wa umaskini kwenye jamii na kaya nyingi Tanzania kwani kunakua na muendelezo wa hali duni kutokana na kushindwa kuongeza ungwe…

Carol Ndosi
Carol Ndosi

Written by Carol Ndosi

🇹🇿 |Development Advocate|#GlobalGoalsTZ Champion|Feminist|MWF ‘16|Social & Biz Entrepreneur @MaMaendeleo @nyamachomafest @bongofesttz @thelaunchpadtz

Responses (1)